Mauaji ya Wachunguzi wa UN, DRC

Wapiganaji nchini DRC Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji nchini DRC

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa huenda wanajeshi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo au wapiganaji wa waasi nchini humo walihusika na mauaji ya wenzao wawili.

Michael Sharp, raia wa Marekani na Zaida Catalan, mwenye uraia wa Uswizi na Chile waliuawa Machi mwaka huu walipokuwa wakifanya utafiti kuhusu hali ya usalama nchini Congo.

Wachunguzi wanasema wenzao hao walipanga kukutana na kiongozi wa wanamgambo, siku moja kabla ya kuuawa.