Asilimia 90 wa wakenya wamesikia na kuona habari bandia

Asilimia 90 wa wakenya wamesikia na kuona habari bandia
Image caption Asilimia 90 wa wakenya wamesikia na kuona habari bandia

Karibu asilimia 90 ya wakenya wameona au kusikia habari za uongo kuhusu uchaguzi mkuu unaokuja, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kote nchini humo.

Utafiti huo uliowahusisha wakenya 2,000 kupitia ujumbe ya SMS mwezi Mei, pia uligundua kuwa asilimia 87 ya wale walipata habari hizo walizichukulia kuwa potovu au bandia.

Zikiwa zimesalia chini ya siku 20 kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu, kumekuwa na habari nyingi potovu kutoka mitandao iliyobuniwa kwa lengo la kupotosha tu.

Utafiti huo pia uligundua kuwa vyombo vya habari vya kitamaduni kama radio viliaminika sana kwa habari.

Facebook na WhatsApp imeorodheshwa kama mitandao ya kijamii iliyo maarufu zaidi ambapo watu hupata habari.