Sudan yaagiza shule za makanisa kufunguliwa Jumapili

Kanisa linalalamika kwamba siku ya Jumapili imekuwa siku huru ya shule za kanisa tangu shule hizo zianzishwe nchini humo. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kanisa linalalamika kwamba siku ya Jumapili imekuwa siku huru ya shule za kanisa tangu shule hizo zianzishwe nchini humo.

Wizara ya elimu nchini Sudan imeripotiwa kutoa agizo kwa shule zote za kanisa kufunga siku ya Ijumaa na Jumamosi na kuendelea na masomo kama shule nyingine siku ya Jumapili.

Kulingana na afisa wa uhusiano mwema wa kanisa la Coptic nchini Sudan mamlaka ilivunja shule ya kikatoliki ya Angola wiki moja kabla ya kuanza kwa utafiti, ikiwaacha wanafunzi 500 wanaotafuta shule mbadala.

Kanisa linalalamika kwamba siku ya Jumapili imekuwa siku huru ya shule za kanisa tangu shule hizo zianzishwe nchini humo.

Kulingana na Wakristo Jumapili ni siku ya kupumzika wakati ambapo Waislamu hupumzika siku ya Ijumaa.

Hatua hiyo inajiri muda mchache kabla ya kiongozi wa kanisa Anglikana duniani kutembelea Sudan