Israel kufunga matangazo ya kituo cha Al Jazeera

The Al Jazeera Media Network logo is seen inside its headquarters in Doha, Qatar June 8, 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Israel kufunga matangazo ya kituo cha Al Jazeera

Israel inataka kufunga ofisi za kituo cha Al Jazeera na kufuta vibali vya waandishi wake, kwa mujibu wa waziri wa mawasiliano nchini humo.

Ayoub Kara alidai kuwa kituo hicho kinaunga mkono ugaidi na kusema kuwa vituo vyote vya lugha za kiarabu na kiingereza vitazuiwa kupeperusha matangazo yao nchini humo.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hivi majuzi aliikashifu Al Jazeera kwa uchochezi.

Al Jazeera imejitetea vikali ikisema kuwa iko huru.

Bwana Netanyahu aliilaumu idhaa ya kiarabu kwa ghasia za hivi majuzi katika eneo takatifu mjini Jerusalem.

Hatua mpya ziliweka na Israel baada ya polisi wawili kuuliwa karibu eneo hilo, hatua zilizosabisha maandamano kutoka na wapalestina na kusababisha Israel kuondoa mitambo ya kutambua chuma.

Mwezi Julai waziri mkuu Netanyahu aliapa kuitimua Al Jazeera kutokana na kile alichokitaja kuwa inachochea ghasia.

Al Jazeera inasema kuwa waandishi wake wa habari walizuiwa kujiunga na mkutano wa wanahabri ambapo tangazo hilo lilitolewa.