Tetesi za soka Ulaya Jumapili 13.08.2017 na Salim Kikeke

Kylian Mbappe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kylian Mbappe

Paris Saint-Germain wamekamilisha usajili wa Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco kwa pauni milioni 173. (The Times)

Real Madrid watawapiku Barcelona katika kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20. (RAC-1)

Manchester United wametupilia mbali dau la Tottenham la kumtaka Anthony Martial, 21. (RMC Sport)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp atataka kumsajili mshambuliaji wa Napoli Lorenzo Insigne, 26, iwapo Philippe Coutinho, 25, atalazimisha kuondoka na kwenda Barcelona. (Sunday People)

Barcelona watarejea Liverpool na dau la pauni milioni 100 kumtaka Philippe Coutinho. (Sunday Express)

Chelsea wiki hii watapanda dau la pili la takriban pauni milioni 25 kumtaka kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, baada ya pauni milioni 15 za awali kukataliwa. (Sunday Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Drinkwater(kushoto)

Real Madrid wamekiri kukata tamaa ya kutaka kumsajili kipa wa Manchester United David De Gea msimu huu. (Sunday Express)

Barcelona wamemsajili kiungo wa zamani wa Tottenham, Paulinho, 29, kwa pauni milioni 36.6 kutoka Guangzhou Evergrande ya China. (Mail on Sunday)

Paris Saint-Germain huenda wakatumia zaidi ya pauni milioni 54.9 kumsajili beki wa Monaco Fabinho, 23. (ESPN)

Kiungo Mjerumani Mesut Ozil, 28, hataki kubakia Arsenal na anataka kulazimisha uhamisho wa kwenda Barcelona. (Don Balon)

Tottenham watamwaga fedha kabla ya dirisha la usajili kufungwa, wakianza na kupanda dau la kumtaka kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. (Sunday Telegraph)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anahoji kwanini wanamfuatilia Ross Barkley, yeye anawataka zaidi kiungo wa Celta Vigo Pape Cheikh Diop, 20, na beki wa Ajax Davinson Sanchez, 21. (Sun on Sunday)

Ajax wamekataa dau la pauni milioni 36.6 kutoka Tottenham la kumtaka Davinson Sanchez, na amepewa mkataba mpya ili kumshawishi asalie Ajax. (De Telegraaf)

Image caption Davinson Sanchez(kushoto)

Chelsea watakuwa tayari kumuuza Eden Hazard, 26, iwapo Barcelona watakuwa tayari kutoa pauni milioni 110. (Diario Gol)

Manchester United wameanza tena mazungumzo na Inter Milan ya kutaka kumsajili winga Ivan Perisic, 28, na wanakaribia kutoa kitita cha pauni milioni 48 wanachotaka Inter. (Sunday Mirror)

Chelsea wana wasiwasi kuwa mshambuliaji wake Diego Costa, 28, amenenepa sana baada ya kwenda likizo ya mapumziko Brazil na huenda ikawa vigumu kumuuza. (Sunday Times)

Diego Costa huenda akapigwa faini na Chelsea kwa kushindwa kurejea mazoezini wiki mbili zilizopita. (Daily Star)

Liverpool wamemuambia Emre Can, 23, kuwa haendi popote licha ya Juventus kujipanga kutoa pauni milioni 23 kumtaka kiungo huyo Mjerumani ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake. (Sunday Mirror)

Kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, hatimaye atakamilisha uhamisho wake kwenda Everton wiki hii, na hivyo kufanya Swansea kumfuatilia kiungo wa West Brom Nacer Chadli, 28, na huenda kusababisha Tottenham kumsajili Ross Barkley, 23, kutoka Everton. (Sunday People)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gylfi Sigurdsson

Meneja wa Everton Ronald Koeman, baada ya kumsajili Gylfi Sigurdsson atataka kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina Nikola Kalinic, 29. (Sunday Express)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Croatia na Fiorentina Nikola Kalinic, 29, anataka kwenda AC Milan. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Antoinne Griezmann, 26, huenda akaondoka Atletico Madrid, iwapo kipa Jan Oblak, 24, atauzwa kwenda PSG. (Don Balon)

Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio, 21, anataka kutumia nafasi ya Arsenal kumnyatia ili apate mkataba mpya Real. (Diario Balon)

Arsenal wamekata tamaa ya kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, na sasa meneja Arsene Wenger anatazama zaidi kupunguza wachezaji asiowahitaji ili kupunguza gharama za mishahara. (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha PA
Image caption Rafael Benitez

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anataka kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25. (Sun on Sunday)

Tukutane baadaye katika BBC Ulimwengu wa Soka ambapo tutakutangazia mechi ya Manchester United v West Ham United.

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.

Mada zinazohusiana