Guterres: Tofauti za uchaguzi zitatuliwe kwa amani Kenya

Antonio Guterres Haki miliki ya picha AFP
Image caption Antonio Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wakenya kwa kupiga kura kwa njia ya amani wakati wa uchaguzi wa kumchagua rais.

Guterres amesema kwa anafahamu kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais na kutangazwa kwa Rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.

Bwana Guterres ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa wanaopinga matokeo ya uchaguzi kutatua tofauti zinazohusu siasa kwa njia ya kikatiba.

Katibu mkuu aliwataka viongozi wa kisiasa kutuma ujumbe ulio wazi kwa wafuasi na kwashauri kujiepusha na ghasia.

Alisema Umoja wa Mataifa unashirinaiaka kwa karibu na Mungano wa Afrika na washikadau wengine, kuhakikisha uchaguzi nchini Kenya umekamilika kwa njia nzuri.