Ilinichukua miaka 45 kuupenda mwili wangu baada ya kuchomeka

Sylvia Mac was badly burned in a childhood accident Haki miliki ya picha Ena Miller

Sylvia Mac amechukua miaka mingi katika maisha yake kukubali makovu makubwa kwenye mwili wake, yaliyotokana na ajali akiwa mtoto. Anaeleza ni kwa nini akiwa na umri wa miaka 48 ameamua kuwa ni wakati wa kuacha kujificha na kuonekana wazi.

Hakuna sehemu yoyote ya mwili wake isiyojkuwa na makovu usipokuwa tu uso wake.

Makovu yangu yanaanzia shingoni kwenda chini hadi kwa makalio, kisha kwenye tumbo kwenda nchini mwa mguu wangu wa kushoto. Kisha kwa mwili wangu wote.

Nilichomeka vibaya sana nikiwa na umri wa miaka mitatu.

Mama yangu alikuwa akichemsha maji kwa sufuria ili tupate kuoga. Kisha alikuwa akimwaga maji hayo kwa beseni nakuiweka ndani ya bafu.

Haki miliki ya picha Hannah O'Beirne

Tulikuwa tunacheza mimi na ndugu zangu na nikakimbia kwenda chumba cha kuogea na kufunga mlango. Tuliambiwa tusiende bafuni. Nilienda huko na dadangu akasukuma mlango, hapo ndipo nilianguka ndani ya beseni yenye maji moto yaliyosababisha nipate majeraha mabaya.

Nililia sana, nikapigwa na mshutuko na mara gari la kubeba wagonjwa likafika

Waliiambia familia yangu kuwa singeweza kunusurika majeraha hayo.

Walinipatiza na nikawa na maombi yangu ya mwisho.

Fahamu yangu ya kwanza nilipata nikiwa kitandani, nikiwa nimefungwa bendeji kuanzia kwa mikono yangu kwenda chini. Ninakumbuka nikiwa na maumivu wakati wote.

Nimefanyiwa mamia ya upasuaji hadi sasa.

Nikikua watu wengi walimuambia mama yangu "Oh, ni mrembo, anapendeza."

Lakini kwenye kichwa changu nilikuwa najiuliza, wanasema nini hawa, 'Mimi ni mrembo,? sio hivyo. Ndani ya nguo zangu nimechomeka.

Wakati wote nilihisi kuwa na sura mbaya, kwa hivyo niliadhirika kisaikolojia na hata kimwili.

Watoto wangeniita maneno tofauti kama vile mchawi na mwenye ngozi ya nyoka. walinikera sana. Niliambiwa sitawai kuwa na mpenzi, sitaolewa na hata sitakuwa na watoto.

Haki miliki ya picha Sylvia Mac
Image caption Sylvia's back was extensively burned in the accident, she has had hundreds of operations since

Kupigwa picha ni kitu macho nilijizuia nacho, hata picha za shuleni. Kwa hivyo ni vigumu kupata picha zangu nikiwa mtoto. Na hata wakati mwingine ningekuwa na fikra kuwa watu walikuwa wakinipiga picha hata kama hawakuwa wakifanya hivyo.

Sikupitia vitu vingi maishani. Sikufanya mitihani , sikuenda kufanyiwa mahojiano ya kazi kwa sababu ya kukosa kujiamini, na hata sikujua ni kwa nini nilikuwa msongo wa mawazo.

Nikiwa kijana kuna hata wakati nilifikiri kuwa kuna siku nitasimama mbele ya basi ili angalau maisha yangu yafikie kikomo.

Haki miliki ya picha Ena Miller
Image caption Sylia (kulia) akiruka kwenda kwa kidimbwi kuogelea

Sitaweza kusema kuwa yalikuwa ni makosa ya mama yangu. Lakini kuna wakati nilifikiri hivyo.

Ilikuwa vigumu kuwa na mpenzi lakini baadaye nikutana jamaa mzuri na tukaongea usiku wote. Nikamueleza kuhusu makovu yangu, na alikuwa rafiki mzuri sana. akasema hatakuwa na tatizo lolote na hilo na kwamba bado nilikuwa mrembo. Nikampenda mara moja kwa sabuba alinikubali. nilihisi vizuri, nimezaa naye watoto watatu na pia nina mjukuu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea