Kenyatta: Tunakaribisha ushirikiano na wapinzani wetu

Rais Kenyatta alimshinda mpinzani wake Raila Odinga kwa asilimia 54
Image caption Rais Kenyatta alimshinda mpinzani wake Raila Odinga kwa asilimia 54

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa wafuasi wa upinzani ambao hadi sasa wamepinga matokeo ya urais ya wiki iliyopita.

Bwana Kenyatta alimshinda mpinzani wake Raila Odinga kwa asilimia 54 ya kura lakini upinzani umetaja matokeo hayo kuwa yasiyo ya kweli

Jana Jumamosi kinara wa muungano upinzani nchini Kenya Raila Odinga, aliwashauri wafuasi wake kususia kazi leo Jumatatu kama njia ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumanne iliyopita.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wafuasi wengi wa Bw Odinga walihudhuria mkutano huo uwanja wa Kamukunji mtaa wa Kibera, Nairobi

Akihutubia wafuasi wake mtaani Kibera, Nairobi kwa mara ya kwanza kabisa tangu kutangazwa matokeo, ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, Bw Odinga alidai kuwa serikali ilikiwa imepanga kuwaua wafuasi wa upinzani kabla ya kutangazwa matokeo.

Hata hivyo Rais Kenyatta amesema kuwa wakenya wamekubali matokeo hayo na wenngi wamerudi kazini.

"Kwa marafiki ambao bado hawajakubali matokeo, tunaendelea kutoa wito kwao, tunaendelea kuomba ushirikiano wao. Ikiwa kuna wale wanaendelea kupinga, kuna njia za kikakatiba.

Image caption Shughuli za kawaida zimeanaa kurejea Nairobi

Pia Kenyatta aliwataka polisi kujizuia lakini akaongeza kuwa serikali haitaruhusu kupotea kwa maisha na kuharibiwa kwa mali.

Waandshii wa BBC sehemu tofauti za nchi wanasema kuwa hali inaendelea kurejea kawaida sehemu nyingi.

Awali katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka kumi iliyopita, alikuwa ametoa wito kwa Bw Odinga kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.