Klabu kupiga kura kuamua tarehe ya mwisho kuhama wachezaji

Gylfi Sigurdsson and Philippe Coutinho (right) Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hatma ya Gylfi Sigurdsson na Philippe Coutinho bado haijatatuliwa

Klabu za kandanda nchini England zinajadiliana kuhusu pendekezo la kufungwa kwa soko la kuhama wachezaji kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Kipindi cha sasa cha kuhama kwa wachezaji kitafikia tamati tarehe 31 Agosti, wiki tatu baada ya kuanza kwa ligi ya Premia.

Kura inatarajiwa kupigwa wakati wa mkutano wa washika dau tarehe 7 Septemba.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp na wa Swansea Paul Clement ni kati ya wale wametaka kuwepo mabadiliko.

Sheria za Fifa zinasema kuwa muda wa kuhamwa wachezaji unastahili kufungwa Septemba mosi .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Virgil van Dijk

Suala hilo limekuwa tatizo kwa baadhi ya wachezaji wa kutegemewa ambao wanatarajiwa kuhama klabu wakimeo Virgil van Dijk wa Southamptom, Gylfi Sigurdsson wa Swansea na Ross Barkley wa Everton

"Hali nzuri ingekuwa iwapo tarehe ya mwisho ya kuhama ingekuwa kabla ya kuanza kwa msimu," Clement alisema.

Tarehe ya mapema ya kufungwa msimu wa kuhama ingetusaidia mwaka huu," amesema Klopp

Mada zinazohusiana