Trump azilaumu pande husika kwa ghasia za Charlottesville

Trump azilaumu pande pinzani kwa ghasia za Charlottesville
Image caption Trump azilaumu pande pinzani kwa ghasia za Charlottesville

Rais Donald Trump wa Marekani amezilaumu tena pande zote kwa ghasia zilizotekea katika maandamano ya Charlottesville, siku ya jumamosi ambapo mwanaharakati anayepinga ubaguzi wa kijamii aliuawa.

Katika mkutano na waandishi wa habari , Rais Trump amesema waandamanaji wa mrengo wa kushoto waliwashambulia kwa makusudi wale waliokuwa wakipinga kuondolewa kwa sanamu.

Kauli hiyo imelaaniwa vikali zaidi na maafisa wa ngazi ya juu wa chama cha Republican.

Image caption Ghasia zilizozuka katika eneo la Charlottesvile

Watu wengine kadhaa pia walijeruhiwa katika katika tukio hilo

Rais wa Marekani alitoa tamko hilo pia siku ya Jumatatu akiyalaumu makundi yenye kujenga chuki likiwemo la Ku Klux Klan na lile la neo-Nazis.