Chapisho la Obama la 'kuvumiliana' lapendwa sana katika historia ya Twitter

Picha ya Obama na watoto wa rangi tofauti Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Picha ya Obama na watoto wa rangi tofauti

Ndio chombo cha mawasiliano kinachpopendwa sana na rais Trump, lakini ni chapisho la mtandao wa Twitter la rais Obama ambalo limependwa zaidi katika historia ya Twitter.

Chapisho hilo ambalo ni la kwanza kati ya matatu lilimnukuu Nelson Mandela na liliandamana na picha ya rais Obama aliyekuwa akitabasamu na kundi moja la watoto wa rangi tofauti.

Limependwa mara milioni 3 zaidi tangu lilipochapishwa mnamo tarehe 13 mwezi Agosti kufuatia shambulio la Charlottesville Virginia.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Watoto wa rangi tofauti wakimwangalia rais Obama

Chapisho hilo lililipita lile la Ariana Grande alipotuma salamu za rambirambi baada ya shambulio la kigaidi la Manchester 'Taught to Love'{Nilifunzwa kupenda}.

Katika machapisho hayo matatu ya mtandao wake wa Twitter, bwana Obama alinukuu mshororo mmoja katika kitabu cha wasifu wa Mandela, The long Walk to Freedom.

''Hakuna aliyezaliwa akimchukia mwengine kwa sababu ya rangi mizizi yake ama hata dini''.

Nukuu hiyo ilisema: Watu wanafaa kujifunza kuchukia, na iwapo wanaweza kujifunza kuchukia pia wanaweza kufunzwa kupenda kwa kuwa mapenzi huja yenyewe katika moyo wa binaadamu kinyume na chuki.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Chapisho la Obama katika mtandao wa Twitter

Picha hiyo inaonyesha ziara ya bwana Obama 2011 katika kituo cha kuangalia watoto katika eneo la Bethesda, mjini Maryland.

Picha hiyo ilipigwa na aliyekuwa mpigia picha wa Ikulu Pete Souza.

Tangu ushindi wa rais Trump , bwana Souza amekuwa akichapisha picha katika Instagram , zinozoonyesha uongozi wa bwana Obama akiufananisha na mrithi wake.