Hakainde Hichilema ameachiliwa huru Zambia

Bwana Hichilema alikamatwa mwezi Aprili baada ya msafara wake kudaiwa kukataa kuuondokea msafara ya rais Edgar Lungu Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bwana Hichilema alikamatwa mwezi Aprili baada ya msafara wake kudaiwa kukataa kuuondokea msafara ya rais Edgar Lungu

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ambaye anakabiliwa na mashataka ya uhaini ameachiliwa huru, kwa mujibu wa chama chake

Bwana Hichilema alikamatwa mwezi Aprili baada ya msafara wake kudaiwa kukataa kuuondokea msafara ya rais Edgar Lungu wakati viongozi hao wawili walikuwa wakielekea kwenye sherehe za kitamaduni magharibi mwa Zambia.

Alidaiwa kuhatarisha maisha ya Rais.

Kiongozi huyo wa chama cha UPND pamoja na wafuasi wake watano wamefunguliwa mashtaka ya uhaini, ambayo ni makosa yasiyolipiwa dhamana kumbatana na sheria za Zambia. Walikana mashtaka hayo.

Taarifa zililuwa zimaiambia BBC mapema kuwa kuachiliwa kwake ni sehemu ya makubaliano yaliyoongozwa na jumui ya ya madola.

Katibu mkuu wa jumuiya ya nchi za madola Patricia Scotland, alikuwa nchani Zambia wiki iliyopita ambapo alikutana na Rais Lungu na bwana Hichilema.

Baadaye alisema kuwa bwana Hichilema ataachiliwa kwa manufaa ya nchi.