Seneta avaa Burqa ndani ya bunge Australia akitaka lipigwe marufuku

Pauline Hanson aliingia katika kikao cha bunge hilo na kukaa chini wakati wa hoja ya chama hicho kupiga marufuku vazi hilo nchini Australia. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Pauline Hanson aliingia katika kikao cha bunge hilo na kukaa chini wakati wa hoja ya chama hicho kupiga marufuku vazi hilo nchini Australia.

Kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha One Nation Party nchini Australia alivalia vazi la Burqa katika bunge la seneti nchini humo.

Pauline Hanson aliingia katika kikao cha bunge hilo na kukaa chini wakati wa hoja ya chama hicho kupiga marufuku vazi hilo nchini Australia.

Mwanasheria mkuu George Brandis ,ambaye ni waziri wa serikali aliishutumu hatua ya bi Hanson na kumpa tahadhari ya kutoingilia mavazi ya makundi mengine ya kidini.

Bwana Brandis alipongezwa na vyama vya upinzani .

''Hapana seneta Hanson, hatutapiga marufuku Burka'', alisema katika taarifa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bi Hanson akiwa amevalia nguo zake za kawaida

Katika taarifa yake bi Hanson alisema kuwa mpango wa kutaka kupiga marufuku vazi la Burqa hadharani ni swala muhimu linalokumba Australia ya kisasa.

Muswada wake wa kupiga marufuku Burqa utajadiliwa katika bunge la seneti baadaye siku ya Alhamisi.