Harry Kane, Alexi Sanchez na Eden Hazard kuwania taji la mchezaji bora

Mshambuliaji wa Tottenhama Harry Kane kuwania taji la mchezaji bora 2017 Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Mshambuliaji wa Tottenhama Harry Kane kuwania taji la mchezaji bora 2017

Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji katika ligi ya Uingereza aliyeteuliwa kuwania taji la Fifa la mchezaji bora mwaka 2017.

Mshambuliaji huyo wa Tottenham atajiunga na Alexi Sanchez , kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard na N'Golo Kante katika orodha ya wachezaji 24.

Mshindi wa mwaka uliopita Cristiano Ronaldo ameteuliwa pamoja na Lionel Messi wa Bareclona na nyota wa PSG Neymar.

Zlatan Ibrahimovic ambaye mara ya mwisho aliichezea Manchester United pia ameorodheshwa.

Washindi wataamuliwa na jopo la wakufunzi wa vilabu na wawakilishi wa vyombo vya habari na mashabiki.

Upigaji kura unakamilika tarehe 7 mwezi Septemba na washindi watatangazwa katika sherehe ya kutoa zawadi tarehe 23 mwezi Okotoba.