Chemsha bongo ya BBC - Fumbo 2

Jaribu kunoa ubongo wako.... Unaweza kufumbua chemsha bongo ya leo kutoka BBC Swahili?

Unaweza kutambua ni nani anasema uongo?

Kila la kheri!

Cups game Haki miliki ya picha Getty Images

Fumbo 2

John anasema Justin ni muongo.

Justin anasema Tom ni muongo

Tom anasema Justin na John wote wawili ni waongo.

Ukichukulia kwamba wote watatu kila wakati kwa pamoja husema ukweli au kila wakati kwa pamoja huhadaa, nani anayesema ukweli?

Teremka chini kupata jibu

Jibu

Justin ndiye anayesema ukweli.

Iwapo Tom anasema ukweli kumhusu John, basi John bila shaka anasema Justin ni mkweli, na kwa hivyo Tom ni muongo.

Iwapo, upande ule mwingine, John ni msema kweli, basi Justin anasema Tom ni mkweli, jambo ambalo tumebaini kwamba si kweli.

Kwa hivyo, ni Justin pekee asemaye ukweli.

Fumbo hili limeandaliwa na Alex Bellos, kupitiaToday Programme.

Mada zinazohusiana