Grace Mugabe akosa kuhudhuria mkutano wa SADC Afrika Kusini

Rais Mugabe na mkuwe Grace Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Mugabe na mkuwe Grace

Mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amakosa kuhudhudia mkutano wa kanda nchini Afrika Kusini.

Grace Mugabe, 52, anataka kupewa kinga ya kidiplomasia baada ya kulaumiwa kumshambulia mwanamitindo nchini Afrika Kusini wiki iliyopita.

Alikuwa ahudhuria mkutano na wake wa marais kwenye mkutano huo wa SADC

Mamlaka zinasema kuwa anasalia nchini Afrika Kusini wakati ombi lake la kutaka apewe kinga ya kidiplomasia likiendelea kushughulikiwa.

Polisi wanataka kumhoji kuhusu madai hayo.

Polisi wameweka ulinzi mkali kwenye mipaka ya taifa hilo kuhakikisha kwamba Bi. Mugabe hatatoroka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gabriella Engels

Mwamitindo Gabriella Engels 20, alimshtumu Bi Mugabe kwa kumpiga baada ya kumpata akiwa na watoto wake wawili wavulana ndani ya chumba kimoja cha hoteli huko Sandton, mtaa mmoja wa kifahari kaskazini mwa mji wa Johannesburg

Bi Engels aliambia BBC kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule aliko mwanawe Bellarmine.

''Tuliendelea kumwambia hatujui aliko...hatujamuona usiku wote...alinikamata na kuanza kunipiga.Nakumbuka nikianguka katika sakafu na damu nyingi katika uso na shingo yangu.Alitupiga akiwa na chuki nyingi'', alisema msichana huyo.

Mada zinazohusiana