Rais Buhari kurudi Nigeria leo baada ya zaidi ya siku 100 Uingereza

Muhammadu Buhari Haki miliki ya picha RAIS WA NIGERIA / BAYO OMOBORIOWO
Image caption Muhammadu Buhari(katikati)

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, atarejea nyumbani hivi leo baada ya kupokea matibabu mjini London Uingereza.

Haya ni kulingana na taarifa iliyotolewa na ikulu.

Bwana Buhari mwenye umri wa miaka 74 amekuwa nchini Uingereza kwa zaidi ya siku 100 akipata matibabu kwa ugonjwa usiojulikana.

Kutokuwepo kwake nchini Nigeria kulisababisha wasiwasi mkubwa katika taifa hilo lionaloongoza kiuchumi barani Afrika.

Uvumi kuhusiana na afya ya Bwana Buhari, umedumu kwa muda mrefu, tangu alipokwenda jijini London kwa matibabu.

Makamu wa Rais Yemi Osinbajo, amekuwa akiiongoza Nigeria muda huu wote Buhari akiendelea na matibabu.

Anatarajiwa kuhutubia taifa jumatatu saa moja asubuhi.

Mada zinazohusiana