Korea Kaskazini yatishia kujibu zoezi la kijeshi la Marekani

Korea Kaskazini imetishia kujibu vikali zoezi la pamoja la kijeshi lililofanywa na majeshi ya Korea Kusini pamoja na yale ya Marekani.
Image caption Korea Kaskazini imetishia kujibu vikali zoezi la pamoja la kijeshi lililofanywa na majeshi ya Korea Kusini pamoja na yale ya Marekani.

Korea Kaskazini imetishia kujibu vikali zoezi la pamoja la kijeshi lililofanywa na majeshi ya Korea Kusini pamoja na yale ya Marekani.

Msemaji wa jeshi kutoka Kaskazini alisema kuwa anatazama kwa makini kile ilichokitaja mchezo wa kivita wa Marekani .

Pyongyanga imetishia kurusha makombora katika bahari ya kisiwa cha Guam ambacho kina kambi kubwa ya wanahewa wa Marekani .

Image caption Rais Kim Jong Un wa Korea kaskazini

Wasiwasi huongezeka wakati wa zoezi hilo la pamoja la kila mwaka, na kwamba hali imezidi kuwa mbaya zaidi baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la masafa marefu linaloweza kushambulia Marekani.

Mwaka uliopita Pyongyang ilijibu zoezi hilo la kijeshi kwa kufanyia majaribio kombora lake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii