Somalia yaonya mpango wa Alshabab kusambaza uranium Iran

Wapiganaji hao wamekua wakichimba madini ya uranium katika mkoa wanaoushikilia
Image caption Wapiganaji hao wamekua wakichimba madini ya uranium katika mkoa wanaoushikilia

Serikali nchini Somalia imeonya kuwa wapiganaji wa Alshabab wana mpango wa kusambaza uranium huko Iran wakipata msaada kutoka Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Somalia Yusuf Garaad amesema kuwa wapiganaji hao wamekua wakichimba madini ya uranium katika mkoa wanaoushikilia.

Mwandishi BBC wa masuala ya usalama Afrika amesema kuwa madai hayo hayajaeleza ni jinsi gani Alshabab wanachimba ama kusambaza madini hayo.

Idara ya ulinzi ya Marekani haijatoa maelezo yoyote.