Kate Middleton ni mjamzito tena

William na Kate Middleton Haki miliki ya picha Reuters

Mke wa Mwanamfalme mtawala wa Cambridge William, Bintimfalme Kate, ana ujauzito wa mtoto wao wa tatu, kasri ya Kensington imetangaza.

Malkia Elizabeth na familia za wawili hao "zimefurahishwa sana na taarifa hizo."

Sawa na katika mimba alizokuwa nazo awali, Bintimfalme huyo anaugua hyperemesis gravidarum, au umito.

Hataweza kutekeleza majukumu yake aliyokuwa amepangiwa kutekeleza katika kituo cha watoto cha Hornsey Road, London baadaye leo.

Catherine anatunzwa katika kasri la Kensington, taarifa kutoka kasri hiyo imesema.

Mwanamfalme William na Bintimfalme Kate wana mtoto mmoja wa kiume, George, na binti mmoja, Charlotte, walio na umri wa miaka minne na miwili mtawalia.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii