Gari 'laingia' ndani ya nyumba England

Eneo la ajali
Image caption Gari hilo liliingia hadi sebuleni na kumjeruhi mwanamume aliyekuwa akipumzika kwenye kochi

Watu wanne walijeruhiwa, watatu kati yao vibaya, baada ya gari kugonga ukuta na kuingia hadi ndani ya nyumba eneo la York nchini Uingereza.

Gari hilo liliwasha moto kwenye nyumba hiyo.

Gari hilo aina ya VW Golf lilifika hadi sebuleni na kumjeruhi dereva, abiria wawili na mwanamume mmoja aliyekuwa akipumzika kwenye kochi.

Sajini Paul Cording wa kikosi cha polisi cha Yorkshire Kaskazini alisema ni "jambo la kushangaza kwamba hakuna aliyefariki".

Mwanamume mmoja ambaye anaaminika kuwa dereva wa gari hilo, ambaye ana miaka 20 hivi, alikamatwa.

Image caption Polisi walisema inashangaza sana kwamba hakuna aliyefariki

Sajini Cording alisema gari hilo ni kama "liliingia ndani ya nyumba hiyo katika barabara ya Rivelin Way, mtaa wa Clifton Moor.

Polisi wameomba walioshuhudia kujitokeza kutoa habari kuhusu gari hilo kabla ya ajali hiyo.

Mada zinazohusiana

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea