Wasafiri maili elfu nane kumuadhibu mkwe wao

Devbir, Jasbir na Bhupinder Kalsi Haki miliki ya picha HILLSBOROUGH COUNTY SHERIFF'S OFFICE
Image caption Devbir, Jasbir na Bhupinder Kalsi (kutoka kushoto kuelekea kulia) vyeti vyao vya usafiri zimezuiliwa.

Wanandoa walisafiri maili elfu 8 , kusaidia ''kumuadhibu'' mkwe wao , polisi wa Florida wamedai.

Jasbir Kalsi, mwenye umri wa mika 67, na mkewe Bhupinder, 62, wanasemekana walisafiri kutoka eneo la Punjab hadi kaunti ya Hillsborough kusaidia , '' kumpa ushauri na nidhamu'' mkwe wao.

Silky Gaind, alipatikana amepigwa na kujeruhiwa na afisa wa polisi siku ya Jumamosi baada ya kupata ujumbe kutoka kwa wazazi wake.

Msichana ajiua kwa sababu ya hedhi India

Wakwe zake na mumewe kwa sasa wanakumbwa na mashtaka kadhaa, ikiwemo ya unyanyasaji.

Babake mkwe, ambaye amekuwa akiwatembelea na mke wake kwa mwezi mmoja hivi, pia wanadai mtoto wao alimshikia kisu mkewe kwenye shingo yake

'Niuwe nife'

Bi Gaind, mwenye umri wa miaka 33, amekamatwa mara kadhaa kabla ya wasimamizi kutoka ofisi za Sheriff katika kaunti ya Hillsborough, kufika nyumbani mwake, kulingana na vyombo vya habari nchini humo.

Hatahivyo hapo awali, familia ilijaribu kuwazuia maafisa kuingia kwenye nyumba hiyo, na iliwalazimu maafisa wa usalama kuagiza maafisa wengine wa akiba , pale bi Gaind alipowaita kumsaidia yeye na mwanawe wa mwaka mmoja.

Siku ya Jumapili, wakati kesi ilipokuwa ikisikizwa, Bi Gaind aliambia jaji , mumewe mwenye umri wa miaka 33 alimuacha katika hali ya wasiwasi na maisha yake.

''Nilikuwa naogopa , kwa sababu usiku wa kuamkia jana aliniambia ataniua , iwapo nitawaita polisi. Angeniuwa, wajua? Aliniambia ingechukua dakika 10 kwa polisi kufika kabla yeye kuniua na kujiua mwenyewe,'' Alisema hivyo kwenye Bay News

WFLA ilimripoti Jasbir Kalsi kwamba amekuwa akikabiliwa na mashtaka ya kutekeleza unyama kwa kutumia kisu, huku mumewe Devbir akishtakiwa kwa kutekeleza unyama kwa kutumia nguvu.

Wote wameshtakiwa kwa mashtaka ya uongo, unyanyasaji wa mtoto na kutowaruhusu maafisa kutuo msaada ili 911 kutekeleza wajibu wao.

Bhupinder Kalsi, alihukumiwa kwa unyanyasaji wa kinyumbani na kutoripoti unyanyasaji kwa mtoto

Mada zinazohusiana