Wanawake 20 wauawa katika njia ya kushangaza Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake 20 wauawa kwa njia ya kushangaza Uganda

Wananchi nchini Uganda wamebaki vinywa wazi kutokana na mauaji kadhaa ya wanawake.

Wanawake 20 wameuawa Kaskazini mwa jiji la Kampala pamoja na wilaya jirani.

Wengi wao wamebakwa na kunyongwa, miili yao imetupwa katika mashamba, vichaka na pia misitu.

Ingawa watu kadhaa wamekamatwa na wengine kufikishwa mahakamani kuhusiana na mauaji hayo, lakini wanawake wengi bado wanaishi kwa hofu.

Siraj Kalyango na taarifa ifuatayo kutoka Kampala.

Mada zinazohusiana