Hasira ya Saudia baada ya mawasiliano ya simu na Qatar

Qatar Airways Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege za Qatar zimepigwa marufuku kuruka katika anga ya mataifa jirani ya ghuba

Saudi Arabia imesitisha majadiliano ya aina yoyote na jirani yake Qatar.

Tangazo hilo la Saudia limejiri muda mfupi baada ya kinachoonekana kuwa ni mwanya katika kuafikiana kwenye jitihada za kutatua mzozo wa kati ya mataifa hayo mawili.

Zaidi ya miezi mitatu iliyopita Saudia na mataifa mengine ya ghuba yalikatiza uhusiano na Qatar --- wakiishutumu kwa kuunga mkono makundi ya wapiganaji jihadi na kuwa karibu mno na Iran.

Lakini usiku wa kuamkia Jumamosi kiongozi wa Qatar, Sheikh Tamim na mwanamfalme wa Saudia, Mohammad bin Salman waliwasiliana kwa simu ambapo walielezea hamu yao ya kufanya mazungumzo.

Hatahivyo, muda mfupi baadaye Saudia imesitisha mazungumzo ya aina yoyote ya ziada.

Walikasirishwa na namna Qatar ilivyoripoti mawasiliano hayo ya simu --- inavyoonekana ni kwasababu vyombo vya habari havikueleza kuwa upande wa Qatar ndio ulioidhinisha mawasiliano hayo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii