Ni kwanini visodo vilivyotumika vinakusanywa India?

Visodo vilivyotengenezwa kwa vitambara India Haki miliki ya picha Dr Atul Budukh/TMC Hospital
Image caption Maafisa wa afya walikusanya visodo vya vitambara vilivyotumika kutoka kwa wanakijiji

Hedhi ni jambo lisilozungumziwa India, kwa hivyo hebu fikiria hisia dhidi ya fikra ya kukusanya visodo vilivyotumika na wanawake wakiwa katika hedhi.

Lakini hilo ndilo walilofanya wahudumu wa afya katika vijiji katika jimbo la magharibi India Maharashtra - ili kutambua uwezekano wa wanawake kuugua saratani ya kizazi.

Zaidi ya robo ya wagongwa wa saratani ya kizazi wanatoka India.

Hatahivyo kuna sababu nyingi kwanini wanawake hawaendi kufanyiwa ukaguzi wa vizazi- ukosefu wa miundombinu na taasisis katika maeneo ya mashinani pamoja na gharama kubwa, na kukerwa na fikra ya kufanyiwa ukaguzi wa ndani ya mwili.

"Wanawake wa mashambani wana haya, wanaogopa ukaguzi huo na huona haina maana," wanasema watafiti walioandika katika jarida la Ulaya kuhusu kuzuia saratani.

Zaidi ya 90% ya wanawake wa mashambani India hutumia vitambara wakati wa hedhi na sio visodo vya kuuzwa madukani.

Watafiti kutoka Tata Memorial Centre na taasisi yakitaifa ya utafiti kuhusu afya ya uzazi India wamegundua kuwa kwa kukagua visodo vilivyotumika wanaweza kutambua uwepo wa kirusi cha human papilloma virus (HPV), kinachosababisha saratani ya kizazi.

"Kizingiti kikuu ya kuidhinisha kwa ukubwa mpango huu wa ukaguzi wa saraatani ya kizazi ni hatari ya kupungua kwa wanawake wanaoshiriki." amesema Dkt Atul Budukh, mtafiti mkuu wa taasisi hiyo.

Kutokana na hilo madakatari wanasema wagonjwa wengi wa saratani hiyo hutambuliwa wakati saratani imekomaa au wakati wakifika hospitali kwa matatizo mengine ya kiafya.

Haki miliki ya picha Dr Atul Budukh/TMC hospital
Image caption Wanasayansi India wanakagua sampuli za visodo katika maabara

Zaidi ya wanawake 500 wameshiriki utafiti huo wa kati ya umri wa miaka 30 na 50, ambao hawana historia ya saratani wana afya nzuri ya akili na mwili na hupata hedhi zao kama kawaida.

Waliwasilisha visodo walivyotumia kwa utafiti huo wa miaka miwili.

Vitambara vya hedhi vilivyokusanywa vilihifadhiwa katika mazingira ya baridi kali na vilitumwa katika taasisi ya ukaguzi kukaguliwa.

Chembechembe za DNA zilitolewa kutoka damu iliokauka na kukaguliwa.

Wanawake 24 waligunduliwa kuwana kirusi hicho cha HPV na walitambuliwa kupokea matibabu zaidi, alisema Dkt Bhuduk.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanawake wachache katika maenoe ya mshinani India hutumia visodo vya kuuzwa.

Watafiti pia walinakili historia yao ya afya ya uzazi wao, vyoo wanavyotumia na vifaa wanavyotumia wakati wa hedhi.

Utafiti huo uligunduwa haja kubwa ya kutoa elimu kuhusu afya na usafi wa sehemu za siri.

Dr Budukh anasema: "kutokana na hali mbaya ya vyoo au ukosefu wa vyoo, wanawake katika maeno ya mashamabni hawana faragha ya kujiosha sehemu zao za siri."

Usafi duni wa sehemu za siri ndio chanzo kikuu cha kuzuka saratani ya kizazi na matumizi ya visodo vilivyotengenezwa na vitambara na kutumika zaidi ya mara moja, inaongeza hatari, utafiti unaonyesha.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii