Taarifa za siri za kampuni ya Apple zafuja

Apple logo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Taarifa za siri za kampuni ya Appla zafuja

Taarifa kuhusu simu mpya za iPhone na vifaa vingine vya Apple ambavyo havijazinduliwa zimefuja.

Mitandao miwili iliruhusiwa kuona aina mbili ya tekenolojia ya iOS kabla ya siku kuzinduliwa.

Taarifa zilizofichuliwa ni za simu ya iPhone X pamoja na ya simu mbili aina ya iPhone 8.

Mwandishi mmoja wa masuala ya teknolojia huo ndio ufujaji mkubwa zaidi katika kampuniya Apple.

Apple inatarajiwa kuzindua kifaa kipya kwenye makoa yake makuu siku ya Jumanne.

Kampuni hiyo yenye makao yake huko California hujitahidi kuficha siri za teknlojia yake hadi wakati wa uzinduzi wa vifaa vyake.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkuu wa Apple Tim Cook

Hata hivyo taarifa kuhusu vigaa vipya vya Apple zlifichuliwa Agosti,

Wakati hilo likionekana kufanyika kimakosa, imedaiwa lakini ufujaji wa hivi majuzi ulikwa wa makusudi.

Hata hivyo BBC imebaini kuwa mtu asiyejulikana alichapisha anwani za iOS 11 zinazofahamika kama golden master (GM) ambazo zilifungua teknolojia katika komputa za Apple.

Apple haijasema lolote.

Hi ni mara ya pili katika kipindi cha mieiz mitatu ambapo kampuni hiyo inajipata katika hali ambapo taarifa zake za siri zinafichuka.

Mwezi Juni sauti ya saa nzima ya mkutano kuhusu njia za kuwazuia wale wanaofichua taarifa zilifichuka kwa mtandao moja wa habari.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Simu za Apple huipa kampuni hiyo faida kubwa

Mada zinazohusiana