Huduma za jamii zitachukua muda kurejea Florida

Marekani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mifumo ya nishati imeharibiwa vibaya

Gavana wa Florida amekuwa akitoa maelezo ya operesheni ya kazi ya misaada inavyofanyika kutokana na hali inayoikabili Marekani baada ya kukumbwa na kimbuga na dhoruba maruufu Irma.

Rick Scott , asema kwamba vipaumbele vya haraka vimeelekezwa katika kusaidia hospitali na kuokoa maisha. Zaidi ya theluthi mbili ya taifa hilo haina nishati ya umeme na bwana Scott amearifu kuwa itachukua wiki kadhaa kurejeshwa kwa ukamilifu wake nishati hiyo.

Moja ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga hicho ni maeneo ya pwani ya mji wa Florida yajulikanayo kama vitovu vya Florida na imearifiwa kuwa itachukua muda kwa wakaazi wa maeneo hayo kurejea katika makaazi yao.

Scott anasema Kuna uharibifu mkubwa , nina matumaini kila mtu alinusurika, ni mambo ya kutisha tuliyoyaona.

Ninajua hali ya taifa letu lakini hasa vitovu vya Florida itachukua muda kurejea katika hali yake ya kawaida, kwakweli kuna uharibifu mkubwa .

''Naelewa kuwa watu walio wengi wanataka kurejea katika maisha yao ya kawaida, najua kila mmoja anataka kuanza upya, nawasihi kuwa na subra, mnapaswa kupata msaada wa haraka katika maeneo yenu, tunapaswa kupata maji tena, tunahitaji huduma zote za kijamii zirejee kama kawaida lakini nasema, itachukua muda nrefu!''