Hotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa

US President Donald Trump at the UN General Assembly in New York, 19 September Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa

Hotuba ya kwanza kuu ya rais wa Mareknai Donald Tump kwenye Umoja wa Mataifa imekosolewa na baadhi ya chi wanachama.

Rais Trump alizitaja nchi zikiwemo Iran akisema pia kuwa Marekani itaiharibu kabisa Korea Kaskazini ikiwa italazimika kafanya hivyo.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Iran alisema, "hotuba ya Trump ni ya wakati ya mikutano ya wanahabari wala sio kwa Umoja wa Mataifa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa

Korea Kaskazini bado haujajibu tisho la Trump kuwa itaharibiwa.

Hotuba ya Trump ilizungumzia zaidi dunia yenye mataifa huru ambayo yana malengo ya kuinua maisha ya watu wao, lakini akatumia muda mwingi akilenga kile alichokija kuwa mataifa yanayoleta matatizo duniani.

Marekani mara kwa mara imeionya Korea Kaskazini kwa majaribio yake ya zana, yanayokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marekani mara kwa mara imeionya Korea Kaskazini kwa majaribio yake ya zana, yanayokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa

Siku ya Jumanne Trump alimkosoa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, akimtaja kuwa mtu wa makombora ambaye yuko katika harakati za kujitia kitanzi.

"Ikiwa Marekani italazimika kujilinda na washirika wake, hatutakuwa na cha kufanya bali tutaiharibu kabisa Korea Kaskazini," aliongeza Trump.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Sweden ambaye alikuwa ameketi katika kikao hicho, alisema kuwa ilikuwa hotuba mbaya, wakati usiofaa na kwa watu wasiostahili.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa

Trump pia aliishambulia nchi ya Venezuela akitaja serikali yake kuwa fisadi na ya kiimla na kuonya kuwa Marekani iko tayari kuichukulia hatua.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Venezuela Jorge Arreaza alipinga kile alichokitaja kuwa vitisho.

"Trump sio rais wa dunia, hata hawezi kuongoza serikaii yake," alisema.

Haki miliki ya picha UN / EVN
Image caption Waakilishi kutoka Israel, Syria, Iran, na Saudi Arabia wakiisikiliza hotuba ya Trump

Akizungumza katika kikao hicho rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, aliteta mkataba wa nyuklia na Iran, akisema kuwa kuuvunja itakuwa makosa makubwa.

Lakini waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alimuunga mkono Bw. Trump. Kwenye hotuba yake aliseka mkataba wa Iran unastali kufanyiwa marekebisho au ufutwe kabisa, na kuonya dhidi ya kukua kwa ushawishi wa Iran eneo la mashariki ya kati.