Wanawake India wasusia zawadi ya Sari waliyopewa na serikali

Wanawake wa india hawakufurahia sari za bei na thamani ya chini walizopewa na serikali kama zawadi
Image caption Wanawake walisikitika kwasababu walikuwa wameahidia kupewa sari za kutengenezwa kwa mikono

Mpango wa kuwapatia zawadi za sari wanawake maskini kama sehemu ya sherehe katika jimbo la kusini mwa India la Telangana sasa umegonga mwamba baada ya wanawake kuanza kukataa mavazi hayo "yenye thamani ya chini''

"Nina wasi wasi vazi hili litadumu zaidi ya siku nne! ," Ganga, ambaye alikuwa tu ndio amepokea sari yake alimueleza mwandishi wa BBC Balla Satish.

Wanawake walisema walisema kuwa wamevunjwa moyo kwasababu hawakupewa Sari zinazotengenezwa na mikono kama walivyoahidiwa na serikali.

Taifa la India linaripotiwa kutumia kitita cha Rupia Bilioni 2.2 swa na $34 kununua mavazi milioni kumi ya sari.

Image caption Kumekuwa na videokwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha wanawake wakichoma moto sari

Mpango wa kutoa sari hizo bila malipo yoyote kwa wanawake, ni mpango wa serikali wa kusherehekea sherehe za tamasha la kitamaduni za watu wa jimbo la , Bathukamma.

Maafisa wanasisitiza kuwa nguo hizo ni za "thamani ya juu", lakini wakaahidi hata hivyo kuwaletea nyingine.

Baadhi ya vyama vya upinzani wametoa wito wa uchunguzi wa kisheria katika kile wanachosema ni " sakata ya sari "wakidai kuwa "sari zenye thamani ya chini " zinadhihirishwa kuwa serikali ilitumia pesa kidogo sana kununua sari kuliko ilivyoahidi.

Image caption Serikali imedai kuwa vyama vya upinzani ndivyo vilivyopanga video hii, kwasababu kuchoma sari "si utamaduni wala tendo'' linalofanyika India

Maafisa walisema awali kwamba wangelinunu Sari kutoka kwa watengenezaji wa jimbo hilo ,jambo ambalo lingeinua sekta ya kutengeneza sari bora zinazotengenezwa kwa mkono.

Lakini walivyogundua kuwa sari zinazoshonwa kwa mikono hazitakuwa tayari wakati wa tamasha, wakaamua kununua zinazotengenezwa viwandani ambazo ni za bei na thamani ya chini.

"tunachukua tu chochote wanachoyupatia ," aliiambia BBC mwanamke mmoja anayeitwa Padma , baada ya kuchukua sari yake kwenye kituo cha mji mkuu wa jimbo Hyderabad,

"Wanadai sari hizi zimetengenezwa kwa mikono ,lakini hapana wanasema tu hivyo," aliongeza.

Video ya mwanamke akichoma rundo la mavazi ya Sari, akidai anataka kujua ni nani atakayevaa sari za "thamani ya chini " imeanza kuenea kwenye mitandao ya kijamii.

Serikali imedai kuwa vyama vya upinzani ndivyo vilivyopanga video hii, kwasababu kuchoma sari "si utamaduni wala tendo'' linalofanyika India.