Trump na vikwazo vipya kwa K.kaskazini

Rais Donald Trump (Kulia) akiwa na kiongozi wa Korea kaskazini Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Donald Trump (Kulia) akiwa na kiongozi wa Korea kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vikwazo vipya dhidi ya mtu mmoja mmoja na makampuni yanayofanya biashara na Korea kaskazini.

Amesema amesaini amri ya Rais, ambayo pia inaipa uwezo Wizara ya Fedha ya nchi yake kuwekea vikwazo mabeki ya kigeni ambayo yanafanya kazi na Pyongyang.

Ameisifia China ambayo amesema imeziagiza benki zake kuacha kufanya biashara na Korea Kaskazini.

Mwandishi wa BBC, katika Umoja wa Mataifa amesema hatua mpya zilizochukuliwa bado hazihusishi katazo lolote lile juu ya usafirishaji wa mafuta kwenda Korea kaskazini, ambapo China inaendelea kupinga.