Viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini watupiana vitisho vipya

A combination photo shows U.S. President Donald Trump and North Korean leader Kim Jong-un Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini watupiana vitisho vipya

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa vitisho vipya kwa Korea Kaskazini kuhusu hutuba kali ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini kweye Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi.

Ri Yong-ho alimtaja Bw Trump kama mtu aliye na matatizo ya akili aliye katika mikakati ya kujitia kitanzi.

Rais wa Marekani alijibu kwa kusema kuwa Bw Ri na kiongozi wa Korta Kaskazini Kim Jong-un hawatakuwepo kwa muda mrefu, ikiwa wataendelea na matamshi yao.

Majabizano hayo mapya yanatolewa wakati ndege za jeshi la Marekani zinaruka karibu na Korea Kaskazini.

Makao makuu ya ulinzi nchini Marekani yanasema kuwa lengo lilikuwa ni kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani uliopo kukabiliana na tisho lolote.

Haki miliki ya picha US Pacific Command
Image caption Majabizano hayo mapya yanatolewa wakati ndege za jeshi la Marekani zinaruka karibu na Korea Kaskazini.

Pentagon ilisema kuwa eneo hilo ndilo eneo mbali zaidi kati ya mpaka wenye ulinzi mkali kati ya Korea mbili ambapo ndege za Marekani zimepitia katika karne ya 21.

Misuko suko imeongezeka hivi majuzi kufuatia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Matamshi ya Bw Yong-ho kwa Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi yaliiga yale yaliyotolewa na Trump siku ya Jumanne kwa UN, wakati alimuita Kim Jong-un kuwa mtu wa makombora aliye kwenye mikakati ya kujitia kitanzi.

Mada zinazohusiana