Merkel aibuka mshindi

Angela Markel Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kansela wa ujerumani , Angela Markel

Kansela wa ujerumani , Angela Merkel ameibuka kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu nchini humo kwa kipindi cha nne. Hata hivyo mamlaka yake imepungua kutokana na uungwaji mkono mdogo ndani ya chama chake chenye mrengo wa kati kutokana na kuimarika kwa chama cha kulia yaani AFD.

Inakadiriwa kuwa chama chenye msimamo mkali dhidi ya wahamiaji cha AFD kinakadiriwa kuwa kwa mara ya kwanza kitashinda asilimia 13 ya viti bungeni.

Mwenyekiti wa chama cha AfD Frauke Petry, anasema Wajerumani wameshuhudia tetemeko la ardhi kisiasa nchini humo.

Image caption Matokeo ya Uchaguzi Ujerumani

Aidha Merkel ameonyesha kutofurahishwa na matokeo ya chama chake. Hata hivyo haya ni matokeo mengine mabaya kuwahi kutokea katika chama chake katika historia ya Ujerumani, tangu yale ya 1933 yaliyo muweka madarakani Adolf Hitler.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii