CHAN: Kenya ilikosea wapi?

Uwanja wa Meru CHAN
Image caption Ujenzi katika uwanja wa Meru mashriki mwa Kenya

Licha ya hatua ya Shirikisho la kandanda barani Afrika - CAF kuipokonya Kenya haki ya kuandaa michuano ya mataifa 16 barani Afrika - CHAN mwakani - hatua hiyo haikushangaza.

Kenya ilishinda haki ya kuandaa mshindano hayo miaka mitatu iliyopita, lakini baadhi wanaona taifa hilo lilijivuta katika kujitayarisha kwa mashindano hayo.

Athari ya uamuzi wa CAF, sio tu kuinyima Kenya haki za kuandaa mashindano hayo, bali pia marufuku iliyoidhinisha dhidi ya maafisa wa michezo nchini, imeendelea kuwa gumzo na kugubika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wakati nchini swali kuu likiwa ni:

Je Kenya imejipata vipi hapa?

Image caption Ujenzi katika uwanja wa michezo Eldoret magharibi mwa Kenya

Makosa yalitokea wapi:

Kuanzia mwanzo Kenya imejikokota, ujenzi wa viwanja umechukua muda mrefu kiasi cha shirikisho la kandanda limeipokonya nchi hiyo haki ya kuandaa mashindano ya CHAN.

Masuali mengi pia yanaulizwa kuhusu maeneo yaliochaguliwa kujengwa viwanja vya michezo.

Kwa mfano, ni utaratibu upi uliofuatwa kuchagua ujenzi wa viwanja hivyo katika sehemu kadhaa huku maeneo mengine hayakuchaguliwa?

Je kuna mkono wa siasa:

Athari za siasa ndio mojawapo ya vyanzo vikuu vya taifa hilo kunyimwa haki ya kuandaa mashindano ya CHAN.

Mwandishi wa BBC Michezo John Nene anataja ukosefu wa usimamazi bora katika sekta ya michezo.

Anatoa mfano wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mnamo mwaka 1996 ambapo siasa ilisababisha mashindano hayo kutoandaliwa Kenya na badala yake yakaishia kufanyika Afrika kusini.

Kenya inatajwa kuwa mojawapo ya nchi zenye uchumi mzuri Afrika mashariki na kati - na haina budi sasa kufuata mifano ya kupigia upatu kama Rwanda na Cape Verde ambazo zimefanikiwa kuandaa mashindano haya.

Haki miliki ya picha Getty Images

Nini Kifanyike:

Yapo mengi tu ya kufanywa kuibadili hali ila mojwapo kuu ni mageuzi ya uongozi katika sekta ya michezo Kenya.

Mwandishi wa BBC John Nene anataja umuhimu wa kuwa na viongozi walio na moyo na ari ya michezo.

Viongozi wanaoongoza kutoka mbele, na watakaoweka siasa duni, mivutano na ukabila kando.

Ilivyo hivi sasa, wadadisi wanatathmini kuwa itaichukua Kenya muda mrefu kuweza kuandaa mashindano hayo ya CHAN kutokana na vigezo vinvyostahili.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii