Waliomuita Nkosazana Dlamini-Zuma kuwa "mke wa zamani wa Zuma" waomba msamaha

Rais Zuma ameoa wake wengi na Bi Dlamini-Zuma alikuwa mmoja wa wake zake watatu hadi Dlamini alipomtaliki mwaka 1998. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Zuma ameoa wake wengi na Bi Dlamini-Zuma alikuwa mmoja wa wake zake watatu hadi Dlamini alipomtaliki mwaka 1998.

Kituo cha taifa cha habari nchini Afrika Kusini kimemuomba msamaha mama anayetarajiwa kuwania urais Nkosazana Dlamini-Zuma, kwa kumuita "mke wa zamani wa Zuma"

Hii ndiyo mara ya pili kituo cha SABC kimemuita mara mbili kwa njia kama hiyo katika kipindi cha miezi miwili.

Mwezi uliopita kituo hicho kilimuita Nkosazana Dlamini-Zuma "mini Zuma".

Mkurugenzi mkuu wa SABC Nomsa Philiso, alisema kuwa matamshi hayo hayakuwa mazuri.

SABC inasema kuwa itafanya uchunguzi na hatakawia kuchukua dhidi ya wale watakaopatikana kufanya makosa hayo.,

Rais Zuma ameoa wake wengi na Bi Dlamini-Zuma alikuwa mmoja wa wake zake watatu hadi Dlamini alipomtaliki mwaka 1998.

Bi Dlamini-Zuma, ambaye ana watoto wanne na Zuma hajaolewa tena.

Mada zinazohusiana