Wauaji wa Kim Jong Nam, kizimbani

Wanawake wanaotuhumiwa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanawake wanaotuhumiwa

Wanawake wawili wanaoshutumiwa kutumia kemikali za neva kumuua kaka wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un- -Kim Jong Nam, wamekana shutuma hizo.

Wamepandishwa kizimbani, katika mahakama ya juu zaidi nchini Malaysia baada ya kesi yao kuanza kusikilizwa.

Wanawake hao Siti Aisyah raia wa Indonesia na Doan Thi Huong kutoka Vietnam, wanashtakiwa kwa mauaji ya Kim katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur mwezi February.

Hata hivyo wamesema walidanganywa wakadhani kuwa wanashiriki mchezo wa maigizo ya kipindi cha Televisheni.

Iwapo watatiwa hatiani, watahukumiwa adhabu ya kifo.