Catalonia yajiandaa kufanya mgomo kulalamikia ghasia za Jumapili

: Protesters hold up flags as they gather outside the "General Direction of the National Police of Spain", offices as Catalonian police officers surround the building on October 2, 2017 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Catalonia yajiandaa kufanya mgomo kulalamikia ghasia za Jumapili

Mgomo mkubwa unatishia kukwamisha shughuli sehemu kubwa za Catalonia kufuatia kura ya maoni yenye utata nchini Uhispania.

Mgomo huo ulioitishwa na vyama vya wafanyakazi huko Catalonia, unalalamikia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulioshuhudiwa wakati wa kura ya maoni ya siku ya Jumapili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wa Catalonia

Uhispania imeitaja kura hiyo ya maoni kuwa iliyo kinyume na sheria. Hata hivyo zaidi ya watu milioni 2.2 walipiga kura.

Lakini mimia ya watu walijeruhiwa wakati polisi wa Uhispania walijaribu kuzuia zoezi hilo kuendelea.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Catalonia yajiandaa kufanya mgomo kulalamikia ghasia za Jumapili

Baadhi ya maafisa walioamrishwa kuwazuia watu wasipige kura walionekana wakifyatua risasi za mipira, wakivamia vituo vya kupigia kura na kuwavuta wanawake kwa nywele zao.

Polisi 3 walijerihiwa siku ya Jumapili, kwa mujibi wa maafisa wa afya huko Catalonia.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamke huyu alipata jeraha la kichwa

mgomo huo wa leo Jumanne utavuruga shushuli za usafiri wa umma, shule na zahahati huko Catalonia.

Klabu maarufu cha kandanda cha Barcelona pia inatarajiwa kugoma, licha ya kuwa hawachezi mechi huku vyuo vya umma na makavazi nayo yakitarajiwa kugoma.

Image caption Ramani ya Catalonia

Mada zinazohusiana