Nissan yazindua kiti cha gari chenye uwezo wa kutambua jasho

Car seat with yellow covering Haki miliki ya picha Nissan
Image caption Nissan yazindua kiti cha gari chenye uwezo wa kutambua jasho

Nissan imeuzindua kiti cha gari chenye uwezo wa katambua jasho la binadamu ambacho kampuni hiyo inasema kuwa kitasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Teknolojia hiyo inayojulikana kama Soak, hubadlisha rangi ikiwa itatambua kuwa dereva atakuwa ameishiwa maji mwilini.

Utafiti wa walia uliofanywa na taasisi za European Hydration Institute na Loughborough University uligundua kuwa madereva wanaoishiwa na maji mwilini huwa na makosa mengi sawa na madereva walevi.

Ngozi hiyo ya kiti iliyoundwa na kampuni moja nchini Uholanzi pia itawekwa kwenye usukani wa gari na viti vya mbele vya gari .

"Hii ni sehemu ya mpango mzima ambao sio tu wa kufuatilia tu gari bali pia dereva." alisema Prof Peter Wells.

Mada zinazohusiana