Ujenzi wa kiwanda cha nyama ya punda wazua ghadhabu Zimbabwe

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ujenzi wa kiwanda cha nyama ya punda wazua ghadhabu Zimbabwe

Makundi ya kupigania haki za wanyama yamegadhabishwa na ujenzi wa kiwanda cha nyama ya punda nchini Zimbabwe ambacho kinatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu, kwa mujibu wa gazeti la serikali Herald.

Kwa taarifa ya pamoja makundi hayo yalisema kuwa ujenzi huo utakuwa wenye athari kubwa kwa idadi ya punda nchini Zimbabwe.

Nyama ya punda ni chakula muhimu nchini China na kupungua kwa punda nchini humo kumewaelekeza wanunuzi barani Afrika.

Ngozi ya punda pia huchemshwa na kutoa kiungo muhimu kwa dawa ya kitamaduni iitawayo ejiao, ambayo hutibu kikohozi na hedhi kwa wanawake ambapo dawa hiyo inaweza kuuzwa dola 388 kwa kilo moja.

Nchi zingine na Afrika zikiwemo Uganda, Tanzania, Botswana, Niger, Burkina Faso, Mali na Senegal, zimepiga china marufuku ya kununua ngozi ya punda wao kwa kuwa mahitaji ni makubwa zaidi.

Mada zinazohusiana