Aliyechapisha habari ya ''nguo za ndani za Bi Grace Mugabe'' aachiliwa

Bi Grace Mugabe Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi Grace Mugabe

Mwandishi wa Zimbabwe ambaye alikamatwa baada ya kuandika habari iliodai kwamba mbunge mmoja aligawanya nguo za ndani za mitumba kwa wafuasi wa chama tawala cha Zanu-PF kwa niaba ya mke wa rais bi Grace Mugabe amewachliwa kwa dhamana ya dola 200.

Kenneth Nyangani pia aliagizwa kuripoti kwa polisi katika mji wa mashariki wa Mutare mara moja kwa wiki.

Amekana mashtaka ya kuchafulia watu majina kufuatia chapisho la habari hiyo katika mtandao mpya wa kibinafsi wa NewsDay.

Maafisa wa polisi katika eneo la Mutare walimkamata bwana Nyangani Jumatatu kwa madai ya kuandika na kuchapisha habari kuhusu ufadhili wa chupi za mtumba zilizodaiwa kutolewa na mkewe rais Robert Mugabe kulingana na mawakili wa haki za kibinaadamu wa Zimbabwe katika taarifa yao.

Mbunge wa chama tawala cha Zanu-PF Esau Mupfumi alisambaza chupi hizo kwa wafuasi wa Zanu-PF mjini Mutare na kusema kuwa bi Mugabe alifadhili nguo kulingana na ripoti hiyo ya NewsDay.

Mada zinazohusiana