Mlinzi aua watoto kwa petrol Brazil

Brazil
Image caption Eneo ambako tukio hilo lilikotokea

Watoto wanne na mwalimu wao mmoja wamekufa katika ajali ya moto nchini Brazil baada ya mlinzi kuanzisha moto katika kituo cha kufundishia watoto wadogo katika shule ya awali.

Mlinzi huyo alirusha petroli kwa watoto hao na kujimwagia pia yeye mwenyewe na kisha kuuwasha moto. Inaelezwa kuw3a mlinzi huyo alikufa akiwa hospitalini kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kwenye ajali hiyo katika mji wa Jana├║ba, katika jimbo la Minas Gerais.

Lengo la shambulizi hilo la moto mpaka sasa halijafahamika wazi, ingawa vyombo vya habari katika mji huo vimearifu kuwa mtu huyo alifukuzwa kazi baada ya kutoka likizo yake ya mwaka kuotokana na hali ya afya yake kuwa mbaya.

Mkanda wa video ilionesha tukio la kutisha jinsi lilivyokuwa nje ya shule hiyo ya awali, huku wazazi wa watoto hao wakionekana kulia kwa uchungu na mshtuko kutokana na tukio hilo wakati walipopokea taarifa kamili ya nini kilichotokea.

Mbali na mshambuliaji huyo kutibiwa hospitalini, watu wengine zaidi ya ishirini wanapata matibabu hospitalini kutokana na majeraha waliyoyapata kwenye tukio hilo.