Mji mkuu wa Ghana Accra wakumbwa na mlipuko mkubwa wa gesi

Incident at Accra's natural gas station
Image caption Mji mkuu wa Ghana Accra wakumbwa na mlipuko mkubwa wa gesi

Mlipuko mkubwa umekumba kitua cha mafuta kwenye mji mkuu wa Ghana Accra, ambapo karibu watu 3 waliuawa.

Mlupuko huo ulirusha moto mkubwa angani na kuwalazimu wenyeji kukimbia eneo la makutano ya Atomic, kaskazini mashariki mwa mji, kwa mujibu wa maafisa.

Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa moja unusu usiku jana Jumamosi. Ripoti zinasema kuwa lori lilokuwa limepeleka gesi lilishika moto.

Watu watatu walithibitiswa kufariki na takriban wengine 30 walijeruhiwa.

Mlipuko wa kwanza uliripotiwa kusababisha mwingine wa pili na moto katika kituo cha petroli.

Kisha moto huo kwenye mtaa wa Legon ukadhibitiwa kwa haraka kwa mujibu wa waziri wa masuala ya ndani Kojo Oppong Nkrumah.

Wenge wa wale waliohamishwa ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Ghana kilicho eneo hilo.

Mwaka 2015 karibu watu 150 waliuawa kwenye moto wa kituo cha Petroli mjini Accra.

Mada zinazohusiana