Duterte aondoa polisi kutoka vita dhidi ya madawa ya kulevya

Rodrigo Duterte Haki miliki ya picha AFP
Image caption Duterte aondoa polisi kutoka vita dhidi ya madawa ya kulevya

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amewaondoa polisi wa nchi hiyo kutoka kwa vita dhidi ya madawa ya kulevya huu harakati hizo zake zikiendelea kukosolewa.

Shirika la kupambana na madawa ya kulevya la nchi hiyo sasa litachukua usukani badala yake.

Polisi wanasema kuwa wamewaua zaidi ya watu 3,850 katika oparesheni za kupambana na madawa ya kulevya tangu Bwa Duterte aingie madarakani mwaka uliopira.

Mwezi Januari, pia aliwatimua polisi kutokana na vita hivyo, akiwalaumu kuwa wafisadi na kisha kuwarejesha tena muda mfupi baadaye.

Polisi hao wanasimamishwa baada ya mwanamke mfanyabiashara raia wa Korea Kusini, kutekwa nyara na kuuawa na polisi wa kupamba na madawa ya kulevya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bw Duterte anakabiliwa na upinzani mkali kutokana na sera zake

Bw. Duterte alachaguliwa mwaka uliopita akiahidi kupiga vita madawa ya kulevya na ufisadi.

Sera zake za kuunga mono mauaji ya kiholela katika vita dhidi ya madawa ya kulevya, zilivutia lawama za kimataifa na lawama ndani ya nchi.

Mwezi Septemba maelf ya watu walifanya maandamano kukosoa vita vyake dhidi ya madawa ya kulevya, licha ya wengine kufanya mikutanao ya kuunga mkono sera za Duterte.

Kesi iliyokumbwa na utata zaidi mwaka huu ni ile iliyomhusu kijana wa kiume amabye aliuawa eneo la Caloocan tarehe 6 mwezi Agosti.

Polisi walisema kuwa kijana huyo wa umri wa miaka 17 alikimbia kutoka kwa polis kisha akawafyatulia risasi, ambapo polisi nao wakamfyatulia risasi.

Wazazi wake walisemaana kuwa hakuhusika kwa visa vya madawa ya kulevya.

Mada zinazohusiana