Marekani yajiondoa Unesco ikilalamikia ubaguzi dhidi ya Israel

Unesco headquarters, Paris (file photo) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani yajiondoa Unesco ikilalamikia ubaguzi dhidi ya Israel

Marekani inajiondoa kutoka shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ikililaumu kwa ubaguzi dhidi ya Israel.

Wizara ya mambo ya kigeni ilisema kuwa itabuni ujumbe wa waangalizi kwenye shirika hilo lenye makao yake nchini Ufaransa kuchukua mahala pa uwakilishi wake.

Mkuu wa Unesco Irina Bokova, alisema kujiondia kwa Marekani ni hatua ya kujutia.

"Kujiondoa kwa Marekani ni pigo kwa familia ya Umoja wa Mataifa," Bi Bokova alisema.

Mwaka 2011 Marekani ilifuta bajeti yake kwa Unesco kupinga hatua yake ya kuwapa wapalestina uanachama kamili.

Rais wa Marekani Donld Trump awali amekosoa kile alichotaja kuwa ni mchango mkubwa wa Marekani kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Marekani hutoa asilimia 22 ya bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa na asilimia 28 kwa shughuli za amani za Umoja wa Mataifa.

Unesco iko katika mikakati ya kumteua kiongozi mpya huku mawaziri wa zamani wa Qatari na Ufaransa, Hamad bin Abdulaziz al-Kawari na Audrey Azoulay wakiwa sako kwa bako kuchukua mahala pa Bokova.

Mada zinazohusiana