Israel yaungana na Marekani kujitoa UNESCO

makao makuu ya UNESCO Haki miliki ya picha AFP
Image caption makao makuu ya UNESCO

Marekani na Israel wametangaza kujitoa ndani ya shirika la UNESCO kwa kile wanachodai chuki dhidi ya Israel.

Idara ya serikali ya Marekani imelalamikia hali ya kuongezeka kwa madai yake,kufuatia kulikatia shirika hilo misaada,miaka sita iliyopita kutokana kufuatia kuipatia uanachama Palestina.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu,ameelezea uamuzi wa Marekani kama ni jambo la kutia moyo na lenye maadili ndani yake.

Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova,amekiri kuwepo kwa hatua hizo.Mwandishi wa BBC anasema uamuzi huo unaendana na msimamo wa rais Trump na jinsi ambavyo amekuwa akibeza kuhusiana na gharama za uendeshaji taasisi za kimataifa na umuhimu wake.