Afrika: Picha za kutoka 6-12 Oktoba 2017
Baadhi ya picha zilizovutia zaidi kutoka barani Afrika na za Waafrika walioko sehemu mbali mbali duniani wiki hii.

Vijana wa Kisomali wakifurahia Ijumaa kwa kupiga mbizi, kucheza na kuogelea mbele ya magofu ya nyumba ya zamani katika pwani ya Hamarweyne, jijini Mogadishu

Nchini Afrika Kusini, Mwanaume aliyevalia mavazi za kitamaduni wanatumbiza watu kabla ya mchuano wa majaribio wa raga kati ya Springboks na All Blacks mjini Cape Town.

Masalio ya mkasa wa moto Jumamosi baada ya lori lililokuwa likibeba gesi kushika moto katika mji mkuu wa Ghana, Accra, na kusababisha mlipuko mkubwa.

Wanamitindo wanaonyesha mavazi yaliyotengenezwa na mbunifu wa nguo Bi Zahui wakati wa maonyesho ya mavazi ya Afrik mjini Abidjan siku ya Jumamosi.

Bara jingine, maonyesho mengine. Raundi hii ikifanyika mjini Lisbon, ambako mavazi ya mbunifu kutoka Angola Nadir Tati yalionyeshwa katika wiki ya kuonyesha mavazi Jumapili.

Mechi ya kandanda ya kufuzu kwa Kombe la dunia 2018 kati ya Misri na Congo Brazzaville iliwavutia mashabiki wengi katika uwanja wa mpira wa Borg El Arab Stadium mjini Alexandria siku ya Jumapili.

Furaha kwa Wamisri, timu yao ilishinda 2-1, na kupata nafasi ya kucheza katika fainali hizo za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miongo miwili.

Wakimbiaji wengine walikimbia wikendi katika mbio za nyika za kilomita 100 nchini Tunisia.
Mohamed el-Morabity mzaliwa wa nchi ya Morocco ambaye alishinda mbio hizo anaonekana hapa akikata kiu.

Siku moja baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne nchini Liberia, wafuasi wa chama cha Coalition for Democratic Change kinachoongozwa na Georgia Weah wanafuatilia matukio katika redio kujua rais wao mpya ni nani.

Polisi wa kupambana na ghasia wakisimama kidete huku wafuasi wa mrengo wa upinzani National Super Alliance (NASA) wakifanya maandamano jijini Nairobi, Kenya siku ya Jumatano.

... na hapa polisi wanawatawanya wafuasi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta waliojitokeza kuwakabili wafuasi wa Bw Raila Odinga.

Mchoro mkubwa katikati mwa mji wa Johannesburg uliochorwa na mchoraji wa grafiti "Falko", sasa ni mmojawepo ya vivutio vya utalii vinayoonyesha mandhari ya mji huo.

Tukisalia na sanaa wacheza dansi ya Ballet kutoka mjini Jo'burg wanajiandaa kwa maonyesho ya mwisho ya Snow White nchini Afrika Kusini 12 October 2017.
Picha kwa hisani ya AFP, EPA, PA na Reuters