Tillerson: Mazungumzo yataendelea na Korea Kaskazini hadi "bomu la kwanza lianguke"

A South Korean marine on exercises on South Korea's Baengnyeong Island, 7 September Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Korea Kusini wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye mpaka

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson, amesisitiza kuwa Donald Trump anataka kutatua mzozo na Korea Kaskazini kwa njia ya mazungumzo.

"Hilo litaendelea hadi bomu la kwanza lianguke," aliiambia CNN.

Vikwazo na mazungumzo , alisema, vimeleta umoja wa kimataifa dhidi ya mipango ya nyuklia ya Korea Kaskazini.

Mwezi uliopita, Bw. Trump alimuambia Bw. Tillerson asitupe muda wake kutafuta mazungumzo na Kim Jong-un.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rex Tillerson anasema Trump anataka kutatua mzozo huo kwa mazungumzo

Wakati wa mahojiano ya leo Jumapili, Tillerson alikataa kuzunguma ikiwa alimuita Bw. Trump mjinga.

Miezi ya hivi karibuni Korea Kaskazjni imekaidi maazimio ya kimataifa na kuendea na majaribio silaha za nyuklia na kurusha makombora kupitia anga ya Japan.

Wadadisi wanasema kuwa taifa hilo liko mbioni kuunda kombora lenye uwezo wa kufika nchini Marekani.

Mada zinazohusiana