Areruya Joseph ashinda mbio za baiskeli za Tour of Rwanda

Areruya Joseph ashinda mbio za baiskeli za Tour of Rwanda
Image caption Areruya Joseph ashinda mbio za baiskeli za Tour of Rwanda

Areruya Joseph Mnyarwanda anayechezea timu ya waendeshabaiskeli ya Dimension Data ya Afrika kusini,ndiye aliyenyakuwa raundi ya kwanza ya mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli ya Tour of Rwanda.

Areruya ametumia muda wa saa tatu na dakika 12 na kumuacha nyuma mwenzake pia kutoka timu ya Dimension Data , Main Kent kwa dakika 1,sekunde 30.

Mbio hizi zinatawaliwa na upinzani mkali baina ya wanabaiskeli kutoka timu za Dimension Data, Rwanda na Eritrea bila kusahau timu ya Tirol Cycling ya Austria anayochezea bingwa mtetezi Valens Ndayisenga kutoka Rwanda.

Kesho shindano kali linatarajiwa katika mbio za umbali wa kilomita 180 kutoka mji wa kusini wa Nyanza hadi mji wa Rubavu kaskazini.

Zaidi ya waendesha baiskeli 70 kutoka timu 15 za mataifa mbali mbali duniani wanashiriki shindano hilo la Tour of Rwanda.

Image caption Waendesha baikeli wa Eritrea

Areruya Joseph Mnyarwanda anayechezea timu ya waendesha baiskeli ya Dimension Data ya Afrika kusini, ndiye aliyenyakuwa raundi ya kwanza ya mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli ya Tour of Rwanda.

Areruya ametumia muda wa saa tatu na dakika 12 na kumuacha nyuma mwenzake pia kutoka timu ya Dimension Data ,Main Kent kwa dakika 1, sekunde 30.

Mbio hizi zinatawaliwa na upinzani mkali baina ya wanabaiskeli kutoka timu za Dimension Data, Rwanda na Eritrea bila kusahau timu ya Tirol Cycling ya Austria anayochezea bingwa mtetezi Valens Ndayisenga kutoka Rwanda.

Kesho shindano kali linatarajiwa katika mbio za umbali wa kilomita 180 kutoka mji wa kusini wa Nyanza hadi mji wa Rubavu kaskazini.

Zaidi ya waendesha baiskeli 70 kutoka timu 15 za mataifa mbali mbali duniani wanashiriki Tour of Rwanda.

Mada zinazohusiana