Mshauri wa zamani wa Trump akiri kudanganya FBI

Michael Flynn
Image caption Michael Flynn

Aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama wa kitaifa wa rais Donlad Trump, Michael Flynn, amekiri kuwa alisema uongo kwa shirika la ujasusi la FBI kuhusu uhusiano wake na Urusi.

Alikiri kusema uongo kuhusu mazungumzo aliyoyafanya na balozi wa Urusi mjini Washington.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinatarajiwa kusema kuwa mkwe wake Trump Jared Kushner ni miongoni mwa wanachama wa ngazi za juu wa kampeni ya Trump waliomwelekeza Flynn kufanya mawasiliano na watu kutoka Urusi.

Flynn anasema atatoa ushirikiano wakati wa uchunguzi kubaini ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016.

Ikulu ya White House inasema kuwa bwana Flynn hajamtaja yeye ila peke yake.

Mada zinazohusiana