Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 05.12.2017

Raheem Sterling Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raheem Sterling

Mshambuliajia wa Manchester City na England Raheem Sterling, 22, atasitisha mazungumnzo kuhusu mkataba mpya huko Etihad hadi baada ya kombe la dunia. (Daily Mirror)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard anaendelea na mkataba mpya pauni 300,000 kwa wiki huko Stamford Bridge kwa matumaini ya kuwavutia Real Madrid. (Times - subscription required)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Luis Suarez

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez anasema kuwa mchezaji mwenzake wa zamani Neymar, ambaye kwa sasa yuko huko Paris St-Germain hawezi kujiunga na Real Madrid. (Marca)

Arsenal wana nia ya kumuuza Theo Walcott, 28, mwezi Januari huku klabu yake ya zamani ya Southampton na West Hama wakimzea mate wing'a huyo wa England. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Rose

Nyota wa zamani wa Juventus Alessandro del Piero, anaamini mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool mjerumani Emre Can, 23, atakuwa bora zaidi katika klabu hiyo ya Italia. (Liverpool Echo)

Mancheseter United wana uhakika kuwa watamsaini mlinzi wa Tottenham na England Danny Rose, 27, kwa pauni milioni 50 aidha mwezi Januari ua msimu ujao. (Daily Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rafael Benitez

Meneja wa New Castle Rafael Benitez anataka paunia milioni 20 mwezi Januari kuweza kuwanunua wachezaji watatu. (Daily Mirror)

West Ham watakabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid kusaini Fyodor Smolov, 27, mshambuliaji wa Krasnodar na Urusi. (Daily Mail)

Real Madrid watajaribu kumsaini kipa wa Bilbao Kepa Arrizabalaga, 23, na mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 24, mwezi Januari. (Marca)

Mada zinazohusiana