Uswizi kurejesha mamilioni yaliyoibiwa Nigeria

abacha
Image caption Kiongozi wa zamani wa Nigeria San Abacha

Serikali ya Uswizi imetangaza kuwa itazirejesha Nigeria dola za marekani milioni 320 sawa na pauni za uingereza milioni 240 zilizoibwa na kiongozi wa zamani Sani Abacha.

Fedha hiyo ambayo ilizuiliwa mwana 2014 na mahakama ya Uswizi baada ya taratibu za kisheria kufuatawa dhidi ya mtoto wa kiume wa Sani Abacha, Abba Abacha.

Zikiwa zimewekwa Luxembourg, fedha hizo ni sehemu ya mabilioni ya Dola yaliyoibwa wakati wa utawala wa Sani Abacha kuanzia mwaka 1993 hadi 1998.

Kurejeshwa kwa 'Kilichoibwa na Abacha' limekuwa jambo la kipaumbele kikubwa kwa Nigeria. Rais Muhammadu Buhari alilitumia suala hilo katika kampeni zake za uchaguzi za mwaka 2015.

Ingawa makubaliano ya kurejesha fedha hizo yalitiwa saini mwezi March, Wizara inayohusika na sheria nchini Nigeria, Benki ya Dunia na Serikali ya Switzerland wamekuwa kiasi wakivutana kuhusiana na masuala ya kisheria

juu ya urejeshwaji wa fedha hizo, anaeleza mwandishi wa BBC Stephanie Hegarty akiwa Abuja.

Makubaliano ya sasa ya kuzirudisha fedha hizo yametiwa saini jumatatu hii na pande zote tatu mjini Washington, jambo ambalo linaweka uhakika kuwa fedha hizi hatimaye zitarudishwa nchini Nigeria.

Pesa hiyo itatolewa kwa awamu katika viwango vidogo vidogo, kusaidia masuala muhimu katika Nigeria chini ya usimamizi wa Benki ya Dunia na ukaguzi wa mara kwa mara.

Kama kiasi cha kwanza kitakachorudishwa hakitatumika vizuri, fedha itakayosalia itazuiliwa. Hii ni kwa nia ya kuzuia fedha hii kuibwa tena.

Mada zinazohusiana